Image
Image

Rais SALVA KIIR adhamiria kutekeleza mkataba wa amani.

Rais SALVA KIIR ameliambia taifa lake kwamba amedhamiria kwa dhati kutekeleza mkataba wa amani uliotiwa saini mwezi uliopita ili kumaliza karibu miezi ishirini ya mgogoro wa kisiasa wa nchi hiyo.
Akihutubia taifa Rais KIIR pia alisema kulikuwa na watu waliokuwa wamejificha ili
kukwamisha mchakato wa amani wa nchi hiyo na hivyo kutaka wananchi waungane naye katika kutekeleza mkataba huo.
Kiongozi wa waasi ambaye ni Naibu Rais wa zamani Bwana RIEK MACHAR pia alitia saini
mkataba huo baada ya shinikizo la viongozi wa Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika,
Marekani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Lakini katika hotuba yake Bwana KIIR alirudia tena wasi wasi wake kuhusu baadhi ya
vipengele vya mkataba huo kama kupunguza majeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba na
uteuzi wa mgeni kufuatilia utekelezaji wake kuwa ni kuingilia uhuru wa nchi.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment