Serena Williams na Novak Djokovic wafuzu raundi ya tatu ya mashindano ya US Open.
Kadri siku zinavyozidi kuyoyoma, mashindano ya mchezo wa tenisi ya Grand Slam ya US Open nayo yanazidi kupamba moto.
Mkali wa kina dada Serena Williams kutoka Marekani alifuzu raundi ya tatu baada ya kumshinda Kiki Bertens kutoka Uholanzi seti 2-0 za msururu wa 7-6 na 6-3.
Mchezaji huyo nambari moja duniani alianza vibaya mechi hiyo lakini baadaye aliweza kukomaa na kufanikiwa kushinda.
Kwingineko kwa upande wa wanaume, mchezaji nambari moja duniani Novak DJokovic kutoka Serbia naye alimshinda Andrea Haider-Maurer kutoka Austria seti 3-0 za msururu wa 6-4, 6-1, na 6-2.
Haya ni baadhi ya matokeo kamili ya mechi za wachezaji walioorodheshwa katika nafasi za juu duniani katika tenisi;
Wanaume:
Novak Djokovic (Serbia) (1) - Andreas Haider-Maurer (Austria): 3-0 (6-4, 6-1, 6-2)
David Ferrer (Spain) [7] - Filip Krajinovic (Serbia): 3-0 (7-5, 7-5, 7-6)
Rafael Nadal (Spain) [8] - Diego Schwartzman (Argentina): 3-0 (7-6, 6-3, 7-5)
Marin Cilic (Croatia) [9] - Evgeny Donskoy (Russia): 3-0 (6-2, 6-3, 7-5)
Milos Raonic (Canada) [10] - Fernando Verdasco (Spain): 3-1 (6-2, 6-4, 6-7, 7-6)
Wanawake:
Serena Williams (USA) [1] - Kiki Bertens (Netherlands): 2-0 (7-6, 6-3)
Belinda Bencic (Switzerland) [12] - Misaki Doi (Japan): 2-1 (5-7, 7-6, 6-3)
Ekaterina Makarova (Russia) [13] - Lauren Davis (USA): 2-0 (6-1, 6-2)
Agnieszka Radwanska (Poland) [15] - Magda Linette (Poland): 2-0 (6-3, 6-2)



0 comments:
Post a Comment