Licha ya Kocha Mkuu wa Azam,Muingereza, Stewart Hall,
kuibuka na ushindi kwenye michezo yake minne mfululizo ya Ligi Kuu Bara, bado
amekiri kuwa hafurahishwi na maamuzi yanayotokea kwenye mechi hizo.
Kocha huyo amefunguka kuwa, mara kadhaa amekuwa haridhishwi
na waamuzi wa ligi hiyo, lakini ameamua kuweka wazi baada ya maamuzi mabovu
zaidi yaliyofanywa kwenye michezo yake miwili ya mwisho dhidi ya Mwadui FC
waliyoshinda 1-0 na wa Mbeya City waliyoshinda 2-1.
Stewart alifika mbali na kusema kuwa muda mwingine huwa
anafikiria labda waamuzi hawapendi kuona Azam inafanya vizuri, ndiyo maana
yanatokea yote hayo na maamuzi yasiyo na haki kwenye mechi zao.
“Waamuzi wamekuwa tatizo sana, kadi nyingi hutolewa hovyo
kwenye mechi zetu lakini pia haki imekuwa haipatikani. Ishu si kushinda mechi
mfululizo, kinachotakiwa ni mpira wa haki na kuchezesha mechi kwa kufuata
sheria na si vinginevyo.
“Kuna muda mtu unaweza kufikiri labda watu hawataki kuona
Azam inafanya vizuri kwenye ligi, maana haiwezekani kwenye mechi mbili za
mwisho mambo yaende tofauti kabisa, hili si zuri kwa kweli, inabidi tubadilike
kwa ajili ya amani na maendeleo ya soka,” alisema Stewart.
Baada ya raundi nne za ligi, Azam inashikilia nafasi ya pili
ikiwa na pointi 12, sawa na Mtibwa Sugar walio nafasi ya tatu pamoja na vinara
Yanga SC.
0 comments:
Post a Comment