Kukohoa ni mojawapo ya njia ya kusafisha koo baadhi ya vitu ambavyo
huweza kumfanya mtu kujisikia kutokuwa na amani kwenye koo lake, sasa
pale anapokohoa ni kama anasafisha.
Lakini kukohoa pia huweza kusababishwa na maambukizi kwenye njia ya
mfumo wa hewa hapo ndipo sasa huwa tunasema mtu amepatwa na shida,
huenda akawa anakohoa kwa sababu ya tatizo ya mzio au allergy ya baadhi
ya vitu fulani fulani,
Moja ya dawa nzuri ya kukabiliana na shida hii ni matumizi ya asali
na juisi ya limao, mtu mwenye tatizo la kukohoa mara kwa mara
anashauriwa kupata mchanganyiko wa asali na limao kidogo ili kuondosha
tatizo hilo.
Hata hivyo, endapo mhusika atakuwa anakohoa mara kwa mara kwa muda wa
wiki mbili hadi tatu mfululizo basi inashauriwa mhusika afike kwenye
kituo cha afya kwa ajili ya vipimo zaidi ili kuweza kubaini endapo
amepata maambukizi ya kifua kikuu na kuweza kuanza matibabu rasmi.
0 comments:
Post a Comment