Image
Image

Asilimia 97 ya zahanati za serikali nchini hazina maabara.

Asilimia 97  ya zahanati za serikali nchini zinadaiwa kuwa hazina maabara hatua inayosababisha baadhi ya wagonjwa hasa wajawazito, watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano  na wazee kupoteza maisha hasa maeneo ya  vijijini.
Akizungumza katika kongamano la kimataifa lililoshirikisha nchi mbali mbali za Ulaya, Asia na Afrika Mashariki lililoambatana na mkutano wa mkuu wa 29 wa Chama cha Wanasayansi za maabara za afya nchini,  kiongozi mkuu wa Sayansi ya Maabara nchini,  JOHN NYIKA amesema utafiti uliofanywa katika maeneo mbali mbali nchini umebaini kuwa ni asilimia 3 tu ya zahanati ndio zenye maabara.
Akielezea tatizo hilo mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,  Dakta  HAJAS SENKORO amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kubainisha kuwa serikali imeanza mchakato wa kuwasomesha wataalama wa Sayansi ya maabara nchini kuanzia ngazi ya cheti.
Amesema wataalam hao watasambazwa  katika maeneo mbalimbali  nchini huku ujenzi wa miundo mbinu ya ujenzi wa maabara za kisasa ikiendelea kufanywa.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment