Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kuzuka hivi karibuni kwa wimbi la machafuko na kukosekana utulivu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na kusema baadhi ya mashambulilio yaliyofanyika ni vitendo vya uhalifu wa vita.
Nchi hiyo ilitumbikia katika wimbi la mapigano ya kidini baada ya mseto wa waasi wa SELEKA wenye Waislamu wengi kupindua serikali mwaka 2013 na kuibuka kwa kikundi cha wapiganaji wa Kikristo kukabiliana na waasi hao.
Katika wiki za hivi karibuni yamezuka mapigano kati ya makundi hasimu ya wapiganaji wa Kikristo na Kiislamu ambapo watu wengi wameuawa na wengine kukimbia makazi yao katika mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka serikali ya mpito kuanzisha uchunguzi kuwatafuta wahalifu hao na kuwafikisha mbele ya sheria.
0 comments:
Post a Comment