Image
Image

Dk.Slaa hatoshiriki tena mikutano ACT- Mwigamba.

Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kimekuwa na mawasiliano na Dk. Wilbrod Slaa, kuhusu uwezekano wa yeye kushiriki katika kampeni za Chama chao kwa lengo la kuendeleza vita dhidi ya ufisadi nchini.
Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Samson Mwigamba anasema kuwa Dk. Slaa ilikuwa afanye nao mikutano ya kampeni katika maeneo tofauti ya Tanzania
"Dr. Slaa alikuwa aanze na Mkutano wa hadhara Mjini Iringa siku ya Jumatano tarehe 7 Oktoba 2015, na baadaye angeendelea na mikutano mingine katika majimbo mbalimbali na kuhitimisha kampeni hizo katika Viwanja vya Mwembeyanga Jijini Dar es Salaam, ambao ndio uwanja ambapo vita dhidi ya ufisadi ilitangazwa rasmi mnamo tarehe 15 Septemba 2007" Alisema Mwigamba
Katibu mkuu huyo wa ACT Wazalendo ameongeza kuwa
"Baada ya tathmini ya kina chama cha ACT-Wazalendo kimejiridhisha kwamba hali ya usalama wa Dkt Slaa ni ndogo sana kwa sasa kutokana na vitisho mbalimbali anavyovipata. Kutokana na hali hiyo ya vitisho dhidi ya usalama wake, chama chetu kimejiridhisha kuwa hakina uwezo wa kumhakikishia Dk. Slaa usalama wake atakapokuwa majukwaani. Kwa kuzingatia maelezo ya hapo juu, chama chetu kimefuta mikutano yote ambayo Dk. Slaa alikuwa aifanye kupitia jukwaa la ACT-Wazalendo. Chama kitaendelea kutambua mchango wake katika harakati za kukuza demokrasia na hasa bidii yake ya kujitoa katika kupambana na ufisadi nchini. Tunamuahidi kwamba chama chetu kitaendeleza vita hii kwa bidii kubwa na juhudi zake kamwe hazitapotea".Amesema Mwigamba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment