Mamia ya wahamiaji wamevuka na
kuingia Slovenia kutoka Croatia leo, baada ya Serikali ya Hungari
kufunga mpaka wao. Wahamiaji 2,500 waliruhusiwa kuingia Slovena
Jumamosi.
Serikali ya Slovenia imesema inaweza kuwashughulikia
idadi kama hiyo tu kwa siku. Hungary ilisema kuwa ilifunga mpaka wake na
Croatia usiku wa KUamkia Jum amosi kwa sababu viongozi wa Muungano wa
Ulaya walishinda kukubaliana juu ya mpango wa kupunguza idadi ya watu
wanaotafuta hifadhi.
Msemaji wa UNHCR, Babar Baloch, alisema kuwa baridi imeongezeka na kutakuwa na changa moto nyingi zaidi.
Amesema
kwa sasa ni msimu wa baridi umefika na idadi ya watu haijapungua. Kwa
hivyo kuna watu wengi zaidi walio katika hali ya kusikitisha na
wanaosafiri.
Msimu wa baridi utaongeza matatizo yao,kwa hivyo kile
tunacho hitaji ni utaratibu tutakaotumia kuwasaidia kutoka mpaka mmoja
hadi mwingine.
Bwana Babar Baloch alisema ameongeza kuwa itakuwa
vigumu zaidi kwao, na kwa hivyo wanatarajia kuimarisha juhudi zao kama
shirika la kuwashughulikia wakimbizi (UNHCR) na kuendelea kuhakikisha
tunawasaidia wakati huu wote mgumu.
0 comments:
Post a Comment