Raia mmoja wa Israel ameuawa katika
mapambano ya kurushiana risasi na kuchomana visu yaliyozuka katika kituo
cha Basi kusini mwa mji wa Beersheva.
Hata hivyo katika mapambano
hayo watu wengine kumi walijeruhiwa wane kati yao wakiwa ni Polisi. Mtu
aliyetekeleza shambulio hilo anadhaniwa kuwa ni raia wa Palestina
ambaye alipigwa risasi na Polisi na kufariki. Inadaiwa kuwa mshambuliaji
huyo alifika kituoni hapo akiwa amejihami kwa Bunduki na visu,ambapo
alifanikiwa kufyatua risasi. Majeruhi mwinmgine ni raia wa Eritrea
ambaye alipigwa risasi na Polisi ambaye alidhani kuwa huyo alikuwa ni
mshambuliaji wa pili.
Zaidi ya 50 wamekufa hadi sasa ndani ya wiki tatu kutokana na machafuko nchini humo.
0 comments:
Post a Comment