Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini NEC imetakiwa kubandika haraka majina
ya wapiga kura vituoni ili wapiga kura wahakiki majina yao mapema kabla
ya siku ya uchaguzi.
Rai
hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
LHRC Dr. Hellen Kijo-Bisimba wakati akiongea na East Africa Radio na
kusisitiza kuwa kama tume ya uchaguzi wakichelewa kutoa majina hayo na
baadaye watu wakakosa kuyaona siku ya kupiga kura na kuikosa haki yao ya
msingi wanaweza kuzusha malalamiko na hata kupelekea machafuko na
Vurugu.
Dr Kijo Bisimba ameongeza kuwa bado kuna tatizo sugu la kampeni za matusi, lugha za kejeli na kashfa dhidi ya wagombea wengine hata kuwatumia wasanii kuwakejeli na kuwatukana wagombea wengine.
Aidha Dr Bisimba amesema kuwa wagombea wanawake hawajawezeshwa vya kutosha na vyama vyao na hivyo wagombea wanawake kushindwa kufanya kampeni vizuri na kushindwa kuwafikia wapiga kura.

0 comments:
Post a Comment