Tume ya mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imevitaka vyombo vya habari
kufuata sheria na taratibu za utangazaji wa matokeo kama zilivyoainishwa
na tume hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam mwenyekiti wa kamati ya
maudhui ya Utangazaji wa TRCA Bi. Margaret Munyagi amesema kuwa lazima
vyombo vyote vya habari nchini kutangaza matokeo toka kwa vyombo vyenye
mamlaka ya kusimamia uchaguzi na vyanzo vya kuaminika tu na si
vinginevyo.
Bi Munyagi ameongeza kuwa kwa wastani vyombo vya habari vingi vimejitahidi kuripoti maudhui mazuri japo bado kuna baadhi ya vyombo havikuzingatia mizani ya habari zao kwa kupendelea baadhi ya wagombe na kutoa habari za upande moja tu.
Kwa upande wake afisa mkuu wa utangazaji Andrew Kisaka amesema kama vyombo vya habari vikikiuka sheria za utangazaji basi wanaweza kupewa Onyo, faini hadi chombo kufungiwa kabisa na kunyang'anywa leseni.

0 comments:
Post a Comment