Image
Image

News Alert:Ajali yaua 2 na kujeruhi 12 Mkuranga.


Watu wawili wanasadikiwa Kufariki dunia wengine zaidi ya 12 kujeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Hiace T575 BTJ na NOAH namaba za usajili T165DET mara baada ya kugongana uso kwa uso katika eneo la kitonga njee kidogo ya jiji la Dar es Salaam Mkuranga mkoani Pwani.
Wakisimulia kwa uchungu mashuhuda hao wa ajali wamesema kuwa sababu kuu walio iona hadi kusababisha ajali hiyo iliyopoteza maisha imekuwa nimwendo kasi hali iliyo sababisha gari hizo mbili kuvaana na kusababisha vifo.
Wamesema vifo hivyo vimehusisha Madereva wa Gari hizo mbili ambapo kutokana na mwendo kasi huo hakuna aliyeweza kujiokoa na hivyo kujikuta wakipoteza maisha kwa wakati mmoja.
Aidha jeshi la Polisi kitengo cha usalama Barabarani limekuwa likiwasihi Madereva kuendesha magari kwa mwendo wa pole ili kunusuru maisha ya abiria na wao wenyewe lakini suala hilo bado linaonekana kuendelea kupoteza maisha yao huku kikubwa kikitajwa kuwa ni mwendo kasi,jambo ambalo limekuwa wimbo kila kona.
Nimekuwekea Video Hapa Tizama,Like Page yetu na kuwa wa kwanza kupata habari.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment