Image
Image

Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu.

Mwanariadha mlemavu nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius ameruhusiwa kuondoka gerezani mwaka mmoja tu baada ya kufungwa jela kwa kosa la kumpiga risasi na kumuuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Aliachiliwa huru Jumatatu usiku badala ya Jumanne kama wengi walivyotarajia. Baada ya kuachiliwa huru, alielekea kwa mjomba wake Arnold Pistorius.
Pistorius ameruhusiwa kukamilisha kifungo chake cha miaka 5, akiwa nyumbani kwake.
Mwanariadha huyo alipatikana hatia mwezi Octoba mwaka ya kumuua bila kukusudia mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Kama sehemu ya msamaha huu bingwa huyo wa zamani wa mbio za walemavu atahitajika kukaguliwa kisaikolojia kila baada ya kipindi fulani na hatawahi kuruhusiwa kumiliki bunduki.
Familia yake imekanusha madai kuwa ameachiliwa mapema ikisema kuwa japo hayumo gerezani angali anatumikia kifungo chake nyumbani.
Msemaji wa familia hiyo amesema kuwa hajapunguziwa kifungo na atatumikia kipindi hicho kwa uadilifu kulingana na sheria za taifa.
Hata hivyo bingwa huyo wa zamani anakabiliwa na hatari ya kurejeshwa gerezani iwapo kiongozi wa mashtaka atafaulu kubatilisha uamuzi wa mahakama ya chini iliyompata na hatia ya kuua bila kukusudia Steenkamp.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment