Msanii wa Hip Hop nchini Tanzania
anayetamba na kibao chake cha Viva Roma Viva,Ibrahim Mussa (Roma Mkatoliki)
amesema anasikitishwa na habari za kufikirika za kufungiwa kwa wimbo wake mpya.
Wiki mbili zilizopita msanii huyo
aliachia kibao hicho ambacho kimekuwa gumzo kubwa mitandaoni na mitaani
kutokana na ujumbe uliomo ndani ya ngoma hiyo iliyo samba zaidi mitandaoni.
Kwa mujibu wa Roma mwenyewe kupitia
ukurasa wake wa Instagram amewataka wataalamu wa Kiswahili kumsaidia juu ya
tungo za nyimbo hizo zinazosemekana kukosa ushahidi kwa kuwa alitumia fasihi.
Eti tunafungia Wimbo wa Viva Roma
Viva kwa sababu hakuna ushahidi katika kitu kilichoimbwa wataalam wa Kiswahili
nisaidieni hapa,ushahidi wa fasihi ni upi? Na ukoje?.
Mdogo wangu amini aliwahi kuimba
miaka mingi iliyopita akasema “Bado Robo Saa Mimi Nife’ hadi leo ni mzima wala
hajafa,sasa Amini alikuwa ana ushahidi gani?
Na kama hadi leo ni mzima je
yumhukumu”alisema Roma.
Tusichanganye kati ya sanaa na
fasihi,siasa na Demokrasia na Uhuru.
Aliongeza kwa kusema Kesi ya Ngoma
hiyo kufungiwa na baraza la sanaa la Taifa(BASATA) anaomba ibaki kama tetesi
tu,maana ushahidi wa barua hakuna ambayo pengine ingeeleza sababuzao kwa marefu
zaidi ya kufungia wimbo huo.
0 comments:
Post a Comment