TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa taarifa yenye mkanganyiko
kuhusu wapigakura ambao wanaruhusiwa kupiga kura na wale wasioruhusiwa
kupiga kura;pamoja na kuruhusu watu wenye vitambulisho vyenye namba
totauti na zile zilizo kwenye Daftari la Kupiga Kura.
Katika taarifa ya Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva, iliyotolewa kwa vyombo vya habari iliainisha makundi ya watu ambao wanaweza
kupiga kura licha ya kasoro kwenye mfumo wa Daftari la Wapiga Kura na
wale ambao hawataweza kupiga kura, hata kama wana vitambulisho vya kupigia kura.
Kipengele cha nne cha taarifa hiyo kinajikanganya na kile cha sita
ambavyo vyote vinawataja watu wenye vitambulisho, lakini majina yao
hayamo kwenye Daftari lakini kimoja (cha nne) kinaruhu watu hao kupiga
kura huku kingine (cha sita) kikiwakataza kufanya hivyo.
kura huku kingine (cha sita) kikiwakataza kufanya hivyo.
Katika taarifa hiyo, kipengele namba nne Lubuva alisema: “Wapiga kura
ambao hawaonekani kwenye mfumo wa Daftari lakini wana vitambulisho
vilivyotolewa na Tume na fomu zao za kuandikishwa kufikishwa Tume na
majina yao kuandaliwa katika mfumo wa orodha bila picha na kupelekwa
kituoni wataruhusiwa kupiga kura.”
Katika kipengele namba sita ambacho ndicho kinachokinzana na cha nne
alisema: “Wapiga kura ambao wana kadi ya kupiga kura lakini hawamo
katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kituoni hawataruhusiwa kupiga
kura.”
MTANZANIA ilimtafuta Jaji Lubuva ili kupata ufafanuzi wa taarifa hiyo ambapo alisema Tume imejaribu kutafuta namna ya kuyafanya makundi hayo yaweze kupiga kura licha ya kuwapo kwa kasoro ndogo ndogo.
MTANZANIA ilimtafuta Jaji Lubuva ili kupata ufafanuzi wa taarifa hiyo ambapo alisema Tume imejaribu kutafuta namna ya kuyafanya makundi hayo yaweze kupiga kura licha ya kuwapo kwa kasoro ndogo ndogo.
“Sisi tuliwafikiria watu hao kuwa wanaonekana wamejiandikisha na wana vitambulisho, lakini tatizo ni kutokuwapo
kwenye Daftari au namba ya kitambulisho kutofautiana wasishindwe kupiga kura kwa sababu inaonekana kabisa wamejiandikisha,” alisema Lubuva.
kwenye Daftari au namba ya kitambulisho kutofautiana wasishindwe kupiga kura kwa sababu inaonekana kabisa wamejiandikisha,” alisema Lubuva.
Hata hivyo, Jaji Lubuva alitoa maelekezo ya kumtafuta Mwanasheria wa NEC, Emmanuel Kawishe, ili aweze kuelezea mkanganyiko huo.
“Maswali yako ni mazuri, ningependa umpigie Mwanasheria wetu
Kawishe umwambie nimeongea na Mwenyekiti kuwa nimekuelekeza kwako ili
unipe ufafanuzi wa maswali uliyoniuliza,” alisema Lubuva.
MTANZANIA ilifanikiwa kumpata Mwanasheria huyo Kawishe ambaye kwa
bahati mbaya hakuweza kufafanua vizuri huku akidai kubanwa na shughuli
nyingi.
Akizungumzia kuhusu mtu mwenye kadi yenye namba tofauti na ya kwenye
daftari kuruhusiwa kupiga kura alisema ndiyo busara za Tume.
Mtanzania: “Kwanini mmeruhusu mtu mwenye kadi yenye namba tofauti na kwenye Daftari kupiga kura?”
Kawishe: “Hiyo ndio busara ya Tume.”
Mtanzania : “Huoni kwamba hilo linatoa mwanya kwa mtu mwenye kadi feki kupiga kura?”
Kawishe: “Ajaribu kupiga na kadi feki aone… nina mambo mengi ya kufanya,” alisema na kukata simu.
Mtanzania ilimpiga tena ili kupata ufafanuzi wa kipengele cha nne
kukinzana na kile cha sita ambapo alijibu: “Watu hao wana tofauti”.
Alipotakiwa kutoa tofauti hizo alijibu haraka: “Jiulize mwenyewe” na kukata simu.
Awali Ofisa wa NEC, Athuman Masesa, katika mahojiano na MTANZANIA, kwamba Tume imekusanya fomu zote zilizotumika wakati wa uandikishaji ili kuhakikisha kila mtu aliyejiandikisha anakuwapo kwenye Daftari.
Alipotakiwa kutoa tofauti hizo alijibu haraka: “Jiulize mwenyewe” na kukata simu.
Awali Ofisa wa NEC, Athuman Masesa, katika mahojiano na MTANZANIA, kwamba Tume imekusanya fomu zote zilizotumika wakati wa uandikishaji ili kuhakikisha kila mtu aliyejiandikisha anakuwapo kwenye Daftari.
Mtanzania ilipotaka kujua kama kutakuwapo na Daftari jingine la
Wapiga Kura lenye majina hayo, Ofisa huyo alisema kitakachofanyika
ni kuhakikisha kila mwenye kadi ya kupiga kura lazima atapiga kura, na
kwamba wametoa
maelekezo hayo kwa wasimamizi wote wa uchaguzi nchini.
maelekezo hayo kwa wasimamizi wote wa uchaguzi nchini.
“Naomba uchukue hii kutoka kwangu kwamba mtu yeyote ambaye ana kadi
halali iliyotolewa na NEC lazima atapiga kura. Kuna mchakato tunaufanya
wa kukusanya zile fomu zote zilizoandikisha wapigakura ili kuangalia
ni majina gani hayapo kwenye Daftari ili yaweze kupelekwa vituoni,”
alisema Masesa.
Hata hivyo alisema watu ambao hawataruhusiwa kupiga kura ni wale
ambao majina yao yapo kwenye Daftari lakini hawana kadi ya kupigia kura.
“Sheria ya Taifa ya Uchaguzi inasema ili mtu aweze kupiga kura kwanza
lazima awe na kadi ya kupiga kura, hivyo unaweza kuona kitu cha kwanza
ni kuwa na kadi, hivyo kama hauna huwezi kupiga kura,” alisema Masesa.
MTANZANIA pia ilizungumza na Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu ya Mpiga
Kura na Habari wa NEC, Clarence Nanyaro, kutaka kujua kama mtu anaweza
kupigia kura rais sehemu yeyote atakapokuwa siku ya kupiga kura.
Nanyaro alifafanua kuwa kila mtu atatakiwa kupigia kura zote (urais,
ubunge na udiwani) katika kituo alichojiandikisha, isipokuwa
wale waliopewa kibali maalumu kutoka NEC.
Alitaja makundi yaliyopewa kibali hicho kuwa ni pamoja na mawakala wa
vyama vya siasa, wasimamizi na wasaidizi wa wasimamizi wa vituo,
wagombea wa ngazi zote za udiwani, ubunge na urais pamoja na watumishi
wa NEC.
Alisema watu walio katika makundi hayo watalazimika kujaza fomu namba
18 na 19 zilizopo katika vituo vya kupiga kura kabla ya kupiga kura.
Alisema watu hao wataweza kupiga kura ya rais wakiwa sehemu yeyote,
lakini kwa upande wa diwani na mbunge lazima awe katika kata au jimbo
alilojiandikishia.
Kuhusu makosa yaliyobainishwa kwenyeDaftari la Kudumu la wapiga Kura,
ikiwamo kuwepo kwa picha na majina yasioendana na wapigakura, alisema
Tume inazifanyia kazi kasoro hizo.
Wakati haya yakijiri, NEC imebandika majina ya wapigakura katika
vituo vyote vya kupigia kura na kuwataka wapigakura waende kwenye vituo
vyao walipojiandikisha kupiga kura ili kuhakiki kama majina yao yapo
kwenye mbao za matangazo au la kwenye vituo husika.
Tangu kutolewa kwa tangazo hilo kupitia njia mbalimbali, zikiwamo
nyumba za ibada, mwishoni mwa wiki iliyopita, wapigakura wamekuwa
wakienda kwenye vituo vyao vya kupiga kura kuhakiki majina yao
kama walivyoelezwa na NEC.
Baadhi ya watu wamekuta majina hayapo kwenye mbao za matangazo. “Cha
kushangaza, unakuta mtu ambaye jina lake halipo, siku alipokwenda
kujiandikisha alifuatana na mke/ mume wake na watoto wao waliofikia
umri wa kupiga kura, lakini baadhi ya majina ya familia hiyo
iliyojiandikisha siku moja hayapo na mengine yapo,” alisema juzi
Frederick
Massawe, Mkazi wa Mbweni JKT (Ndege Beach), nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema, kwa mfano, katika kituo cha kupigia kura cha New Era Primary & Sekondary, Mtaa wa Malindi Estate, kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam juzi, watu walikwenda kwenye kituo hicho na kukuta majina yao hayapo wakati walijiandikisha katika kituo hicho hicho na wana vitambulisho vya kupiga kura vilivyotolewa na NEC mahali hapo.
Alisema, kwa mfano, katika kituo cha kupigia kura cha New Era Primary & Sekondary, Mtaa wa Malindi Estate, kata ya Mbweni jijini Dar es Salaam juzi, watu walikwenda kwenye kituo hicho na kukuta majina yao hayapo wakati walijiandikisha katika kituo hicho hicho na wana vitambulisho vya kupiga kura vilivyotolewa na NEC mahali hapo.
0 comments:
Post a Comment