Image
Image

Uganda kuondoa jeshi lake Sudan Kusini.

Uganda itaanza kuondoa majeshi yake Sudan Kusini ifikapo mwishoni mwa juma.
Kiongozi moja wa kijeshi ameiambia BBC kuwa japo mkataba wa amani uliowekwa sahihi na pande zote hasimu zilipendekeza hilo lifanyike mwishoni mwa juma, vikosi vya NRA vitaanza kuondoka karibuni.
Kamanda huyo anasema kuwa hatua hiyo imetokana na haja ya kuundwa kwa jeshi la muungano wa mataifa ya kieneo yaliyopaswa kuchukua pahala pao nje ya mji wa Juba.
Jeshi hilo la Uganda liliingia Juba yapata miaka miwili iliyopita kwa mwaliko wa rais Salva Kiir.
Japo wameshurutishwa kuondoka wadadisi wa maswala ya kiusalama na uhusiano wa kimataifa wanakubali kuwa kuwepo kwako viungani mwa jiji hilo kuu la taifa hilo kumesaidia kudhibiti hali ya usalama.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment