Kiongozi mkuu wa upinzani Afonso
Dhlakama, ametangaza mpango wa kuanzisha tena upya mazungumzo na serikali hivi
karibuni katika mji mkuu wa Maputo nchini Mozambique.
Kituo cha redio cha
Mozambique kiliripoti kwamba Dhlakama aliagiza wanachama wake kufanya
mazungumzo na serikali wakati alipokuwa akihutubia mkoani Sofala.
Hapo awali, Dhlakama
aliwahi kuamuru wanachama wa upinzani kususia mazungumzo yaliyopangwa kufanyika
mwezi Agosti kwa kudai kwamba serikali ya FRELIMO inakana kuwatimizia masharti
yao.
Baadhi ya masharti ya upinzani ni
kutaka kugawana mamlaka na serikali jeshini na katika idara za vikosi vya
usalama.
Kwa upande mwingine,
rais wa Mozambique Filipe Nyusi pia alitoa maelezo na kuthibitisha uamuzi huo
wa kuanzisha tena upya mazungumzo na upinzani katika siku zijazo.
Mazungumzo hayo
yatajumuisha vyama vingine vya kisiasa, mashirika ya umma pamoja na makundi ya
kidini nchini humo.
0 comments:
Post a Comment