Vijana wametakiwa kutokubali kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa kwa maslahi ya watu wachache huku hao wanaowatumia wanasonga mbele katika maendeleo na wao wanazidi kurudi nyuma.
Rai hiyo imetolewa na Mke wa Rais, Mama SALMA KIKWETE alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kijiji cha Kikomolela kilichopo jimbo la Mchinga na mtaa wa Likotwa, Jimbo la Lindi mjini waliohudhuria kampeni ya kuwanadi wagombea wa nafasi za udiwani, ubunge na urais kupitia Chama Cha Mapinduzi.
Mama KIKWETE ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi kupitia wilaya ya Lindi Mjini amesema kuna baadhi ya wanasiasa wanawatumia vijana kufanya vurugu ambazo hazina faida katika jamii zaidi ya kuleta hasara kwani wanaharibu miundombinu ikiwa ni pamoja na barabara, majengo na hivyo kurudisha maendeleo nyuma.
Kuhusu uchaguzi aliwaomba wananchi wote wa maeneo hayo wakiwemo wanachama wa vyama vya upinzani kuwachagua wagombea wa Chama cha Mapindui ambao watazidi kuwaletea maendeleo kwani Serikali ya CCM imefanya mambo mengi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za afya, elimu, maji na barabara.

0 comments:
Post a Comment