Image
Image

Watoto 37 wenye matatizo ya moyo wafanyiwa upasuaji Muhimbili.

Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Godwin Shirau akizungumza na waandishi wa habari kuhusu matatizo mbalimbali ya moyo.
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) kupitia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (Jakaya Kikwete Cardiac Institute  (JKC) imefanikiwa kuokoa zaidi ya Shilingi mIlioni 800 baada ya kuwafanyia upasuaji wa moyo watoto  37 wenye matatizo ya moyo .
Operesheni hiyo imefanyika kuanzia Oktoba  10 hadi 19 mwaka huu kwa kushirikisha timu ya wataalam  18 kutoka nchini Italy na  Marekani  pamoja na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kutoka taasisi hiyo.
 Kaimu Mkuu wa taasisi hiyo Profesa Mohamed Janabi amewaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kwamba  endapo wagonjwa hao wangetibiwa nje, kila mmoja yangegharimu kati ya Dola za Kimarekai 10,000 hadi 15,000, gharama ambazo Watanzania wengi hawawezi kuzimudu
Kwa mujibu wa Profesa Janabi,  changamoto inayowakabili ni upatikanaji wa damu  na upungufu wa watalaam.
Alifafanua kwamba hivi sasa kuna orodha ya watu 500 ambao wanasubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo, na kwamba desemba mwaka huu, wanatarajia  kupokea wagonjwa wenye matatizo ya moyo  kutoka nchini Zambia.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Moyo cha Watoto, Dk. Edwin Shiran amesema watoto 17 wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua na wengine 20 wamewekewa kifaa maalum kwa ajili ya kuziba matundu na kuzibua  mishipa ambayo  imezibana  na kwamba kati ya hao watoto wawili wametokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Tangu Januari mwaka huu tayari wamekwishafanyiwa upasuaji wa moyo watoto 122 na watu wazima 132 .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment