Hatimaye Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro
imemuachilia huru kiongozi wa taasisi na jumuiya za kiislamu nchini Sheikh
Ponda Issa Ponda.aliyekuwa akikabiliwa Mashitaka matatu aliyokuwa anadaiwa
kuyatenda Agost 2013 ambapo alikuwa akishitakiwa kutoa maneno ya uchochezi
dhidi ya dini nyingine na kushawishi watu kutenda kosa.
Hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Mery Moyo amemuachia
Sheikh Ponda huru baada ya kutoridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa
Mashtaka ikilinganishwa na hati ambayo iliyokuwa imemfungulia mashtaka awali.
Awali hakimu moyo alisema kwamba Sheikh Ponda alikuwa na
mashtaka matatu shitaka la kwanza lilikuwa ni kutotii amri ya awali ya Mahakama
na hivyo kuendelea kutoa mihadhara,Kushawishi watu kutenda kosa na shitaka la
mwisho kuumiza imani ya dini zingine lakini ushaidi uliotolewa mahakamani hapo
kwa mujibu wa hakimu moyo ulikuwa unazungumzia zaidi maneno ya uchochezi
tofauti na maelekezo ya haki ya mashtaka ambayo yenyewe ilipelekwa mahakamani
hapo kuwa Sheikh.Ponda alikuwa akifanya mkusanyiko usio halali.
Upande wa mashitaka haukuweza kubadili chochote wakati
shitaka lilipokuwa likiendelea hii ikiwa ni kwa mujibu wa Sheria,hivyo makosa
aliyokuwa nayo kuonekana hayagusi ile hati mashitaka iliyokuwa ikizungumzia
kufanya mkusanyiko usio halali.
Sheikh Ponda alikuwa akitetewa na mawakili Juma
Nasoro,Abubakar Salim na Bartholomeo Tarimo,ambapo katika kesi hiyo upande wa
mashtaka ulikuwa ukiwakilishwa na wakili wa serikali mwandamizi Benard Kongola,
Sunday Hyera na george Mbalasa.
Endelea kufuatilia taarifa zetu kila zinapotufikia,Like Page yetu kupata habari zaidi.
0 comments:
Post a Comment