Wananchi wa baadhi ya
vijiji vinavyokabiliwa na tatizo
hilo wamesema pamoja na serikali
kuwapatia ruzuku bado ni kubwa kutokana
na uweza mdogo wa kubuni miradi
inayoweza kuwa endelevu.
Aidha wananchi hao
wameiomba serikali kutumia wataalam wake
kuangalia upya namna ya kupata
ufumbuzi wa kudumu ukiwemo wa kuziba mianya inayochangia
kuongezeka kwa umaskini badala ya
kuendelea kupunguza makali.
Wakizungumzia changamoto
hiyo walipokuwa wanazindua awamu
ya tatu ya mpango wa kuzisaidia kaya maskini katika wilaya ya monduli baadhi
ya viongozi na
watendaji wa serikali wa mkoa wa Arusha wamesema zaidi ya
shilingi bilioni 1.7 zimetengwa kupunguza makali ya
tatizo hilo ambapo wilaya ya Monduli yenye
kaya zaidi ya
milioni 6,242 imetengewa milioni .
Mkuu wa mkoa
wa Arusha Bw.Felexs Ntebenda amezitaka idara zinazohusika
kuendelea kuwatambua wananchi wanaokabiliwa
na hali mbaya ili serikali
iweze kuchukua hatua
na amesema hakutakuwa na huruma
na yeyote atakayedhubutu kutumia
fedha zinazotolewa kinyume na
utaratibu na amewaomba
wananchi kutoa ushirikiano.
0 comments:
Post a Comment