Baada ya sintofahamu iliyokea siku za hivi karibuni
kwa zaidi ya wafanyakazi zaidi ya 400 wa Uchumi Supermakert kutojua hatima yao
ya kikazi kutokana na wahusika wa maduka hayo kuyafunga na kuondoka bila wao
kulipwa marupupu yao,Hatimaye wafanyakazi hao wamepaza Sauti na kuiomba
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais.John Pombe Magufuli kuweza
kuwasaidia kusudi walipwe fedha zao wanazo zidai Uchumi SuperMakert jijini Dar
es Salaam.
Wakizungumza wakati wakiwa wamekusanyika kwenye
makao makuu ya duka hilo yaliyopo katika jengo la Quality Center jijini Dar es
Salaam wamesema kuwa wanapata shida bila kujua hatima ya malipo yao kuwa ndio
yamezikwa ama la ama watayapata ikizingatiwa ni miezi miwili sasa hawajalipwa
hali ambayo wameiomba serikali ya awamu ya tano inayoenda na kauli mbiu ya hapa
Kazi tu kuwa itawasaidia.
Kufungwa kwa Maduka hayo ya Uchumi ni kile
kilichokuwa kikielezwa kuwa ni Matatizo ya kifedha yaliolazimu Uchumi kufunga
baadhi ya maduka yake nchini Tanzania, na Uganda kutokana na kuingia hasara
katika biashara hiyo pia.
Katika Mazungumzo yake wakati wa kufungwa kwa Ofisi
hizo za Uchumi Ofisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi Dk.Julius Kipng’etich alisema kuwa
Bodi hiyo imeamua kufunga vitengo vya kikanda ili kuimarisha shughuli zake
nchini Kenya baada ya kupata hasara.
“Maduka yetu ya Uganda na Tanzania huchangia
asilimia 25 tu ya gharama za uendeshaji,Matawi hayo mawili hayajapata faida
yeyote kwa zaidi ya miaka mitano iliyopita jambo linalochangia shughuli zetu
kuyumba”Alisema Dk.Julius Kipng’etich.
Hata hivyo wakati wa Mgomo wa wafanyakazi wa Uchumi
wa kulipwa Marupurupu yao pia nao wasambazaji wa bidha katika maduka hayo nao
waliungana na wafanyakazi hao walipwe madeni yao.
0 comments:
Post a Comment