MKANDARASI aliyepewa zabuni ya ujenzi wa mtaro wa maji uliosababisha
mafuriko katika eneo la Buguruni kwa Mnyamani Machi, mwaka huu,
ameutelekeza.
Mtaro huo ambao ulisababisha watu kuishi katika mazingira magumu,
baada ya kuziba na maji kuingia kwenye makazi yao, ulimfanya Rais Jakaya
Kikwete kufika eneo hilo na kutaka baadhi ya nyumba zivunjwe.
Akizungumza na MTANZANIA, Msemaji wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu,
alisema mkandarasi huyo ambaye alimtambua kwa jina moja la Rozeka
aliondoka eneo la mradi bila kukabidhi.
“Manispaa itamwandikia barua ili hatua za kisheria zifuatwe, ikiwa ni
pamoja na kusitisha kandarasi yake kwa mujibu wa mkataba wake,” alisema
Tabu.
Alisema katika mradi huo unagharimu Sh milioni 200, hadi sasa mkandarasi huyo amelipwa Sh milioni 80.
Akizumgumza na MTANZANIA, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mnyamani,
Abdallah Mng’ae, alisema wao kama wakazi wa eneo hilo, wana hofu ya
kukumbwa na mafuriko kwa kuwa ujenzi wa mtaro huo haujakamilika.
“Ahadi ya rais haijatekelezwa, hadi sasa mkandarasi haonekeni eneo la kazi na ujenzi umesimama,” alisema Mng’ae.
Alisema kuna taarifa kuwa mvua za el-nino zitakazoanza kunyesha hivi
karibuni, huenda zikasababisha maafa makubwa kama ujenzi huo utaendelea
kusimama.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment