Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damiani
Lubuva ametangaza majina ya vyama vilivyokidhi vigezo kikatiba na kisheria
angalau kupata asilimia 5% katika uteuzi wa wabunge viti maalum.
Lubuva amesema katika uteuzi huo CCM viti 64,Chadema Viti
36,CUF Viti 10.
Amesema kuwa kwa mujibu wa Ibara ya 66(1)(b) na ibara ya
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 ikisomwa kwa pamoja na
kifungu cha kutangaza viti Maalumu vya wabunge wanawake visivyopungua asilimia
30 ya wabunge wote.
Pia amesema kuwa kwa mujibu wa uamuzi wa Serikali wa Mwaka
2010 idadi ya wabunge wanawake wa viti maalumu iliongezwa na kufikia asilimia
40,ambapo kwa uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2015 Viti maalum ni 113 (Miamoja kumi
na tatu).
Hata hivyo amebainisha kuwa kutokana na kuwepo majimbo 8
ambayo hayakufanya uchaguzi basi mgawanyo wa Viti Maalum kwa sasa itakuwa 110.
Lubuva ameongeza kwa kusema kuwa katika mchakato huo viti 3
vilivyo baki vitagawanywa baada ya kufanyika kwa uchaguzi katika majimbo hayo.
Aidha amesema kuwa majina ya wabunge wa viti maalum
yatapatikana katika vyama husika kwa mujibu wa orodha iliyowashwa tume na kila
chama ili tume hiyo iweze kufanya uteuzi.
0 comments:
Post a Comment