Rais Barack Obama wa Marekani amewawekea vikwazo viongozi wanne wa
Burundi akiwemo waziri wa usalama Alain-Guillaume Bunyoni kwa kubeba
jukumu la machafuko yanayoikumba nchi hiyo tangu Aprili mwaka huu.
Vikwazo hivyo vinawahusu viongozi wawili wa serikali mjini Bujumbura
pamoja pia na madhamana wawili wa njama ya mapinduzi ya kijeshi
yaliyoshindwa mwezi may mwaka huu.
Tangazo hilo limetolewa wakati waziri wa mambo ya ndani wa Burundi
ametangaza kusitishia kwa muda shughuli za mashirika kumi ya
kiraia.Mashirika hayo yalikuwa mstari wa mbele miongoni mwa wale
waliokuwa wakipinga mhula wa tatu wa rais Nkurunziza.Yanaandamwa na
viongozi wa serikali kwa madai ya "uasi" na wengi wa viongozi wa
mashirika hayo wamekimbilia uhamishoni.
Vikwazo vya rais Obama-vinavyowapiga marufku viongozi hao wa Burundi
kuingia nchini Marekani na mali zao kuziwiliwa-vimefuatia vile
vilivyotangazwa mapema mwezi uliopita wa October na Umoja wa ulaya.
"Haviwahusu wananchi wa kawaida wa Burundi",bali baadhi ya watu
serikalini wanaochangia kupalilia ghasia,kudhoofisha taasisi za
kidemokrasi na kujibebesha jukumu la visa vinavyokwenda kinyume na haki
za binaadam" taarifa ya ikulu ya Marekani imesema.
Marufuku yanamhusu pia mkuu wa zamani wa vikosi vya wanajeshi.
Miongoni mwa waliotajwa kuwekewa vikwazo hivyo ni pamoja na naibu
mkurugenzi wa polisi ya taifa Godefroid Bizimana ambae pia ametajwa
katika orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Umoja wa Ulaya.Kwa mujibu
wa serikali mjini Washington,Godefroid Bizimana ndie aliyeongoza
opereshini za polisi kukandamiza maandamano ya amani ya upande wa
upinzani na kutumia nguvu kupita kiasi.
Mwengine ni Godefroid Niyombare,aliyekuwa kiongozi wa idara ya upelelezi
na pia kiongozi wa zamani wa vikosi vya jeshi,pamoja na waziri wa
zamani wa ulinzi Cyrille Ndayirukire.
Jenerali Niyombare ndie aliyeongoza njama ya mapinduizi yaliyoshindwa
mwezi may uliopita na tangu wakati huo amekimbia akiahidi kumpindua rais
Nkurunziza.
"Burundi inakurubia kutumbukia katika janga la maafa,lakini kuna njia
moja ambayo viongozi wanaweza kuitumia kupata ufumbuzi wa
kisiasa"amesema msemaji wa baraza la usalama wa taifa nchini Marekani
Ned Price.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa akosoa uamuzi wa kupigwa marufuku mashirika ya kiraia.
Mjini Bujumbura kwenyewe,shughuli za mashirika muhimu ya kiraia
zimepigwa marufuku."Hatua hii inamaanisha moja kwa moja kwamba mashirika
yasiyomilikiwa na serikali yamepigwa marufuku kuendesha shughuli
zao-hadi mahakama itakapoamua" afisa mmoja wa wizara ya mambo ya ndani
ambae hakutaka jina lake litajwe.Mashirika hayo kumi yaliyopigwa
marufuku yanalenga shughuli zake katika kupigania haki za
binaadamu,kupambana na rushwa na kuwapatia misaada kwa watoto.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelaani uamuzi huo.Mshauri
maalum wa katibu mkuu nchini Burundi amewasili jana mjini Bujumbura na
amepangiwa kuzungumza na viongozi wa nchi hiyo kabla ya kuwasilisha
ripoti yake kuambatana na azimio la baraza la usalama kuhusu Burundi
lililopitishwa novemba 12 iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment