Serikali ya Uholanzi imeanza mchakato wa kusaidia wadau wa uzalishaji wa bidhaa za maziwa katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania kwa kuwajengea uwezo wa kukuza uchumi kupitia sekta hiyo na kuachana na dhana ya kufuga kwa mazoea.
Hayo yameelezwa na wakufunzi kutoka Uholanzi na Tanzania wa mafunzo ya wadau yaliyoshirikisha wawakilishi wa nchi za Kenya, Misri, Zimbabwe,Uuganda, Ghana pamoja na wenyeji Tanzania .
Wamesema nchi za Afrika bado zimekuwa zikikabiliwa na tatizo la kufuga kwa mazoea badala ya kuipa umuhimu sekta ya ufugaji ambayo inakuza pato la taifa na mtu mmoja mmoja.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Sekta ya Mifugo nchini DR.JULLIUS BWIRE amesema mbali na changamoto hizo Shirika la Chakula Duniani FAO limebaini kuwa kwa kila Mtanzania anakunywa maziwa lita 45,000 chini ya kiwango cha lita 200,000 kilichowekwa na shirika hilo kwa ngazi ya kimataifa.
Home
News
Serikali ya Uholanzi imeanza mchakato wa kusaidia wadau wa uzalishaji wa bidhaa za maziwa katika nchi za Afrika ikiwemo Tanzania.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment