Akizungumza baada
ya kuongoza zoezi
hilo lililoanza alfajiri
kaimu mkuu wa
mkoa wa arusha
Bw.Fadhili Nkurl amesema zoezi
hilo ni endelevu
na ni wajibu wa kila
mmoja kufanya usafi katika
eneo lake na amewataka
watendaji wa jiji
kuhakikisha kuwa yeyote
anayekaidi anachukuliwa hatua.
Bw.Nkurl pia amemtaka
mkurugenzi wa jiji kuhakikisha kuwa
watendaji wanaosimamia idara ya usafi wanatimiza
wajibu wao wakiwemo
wanaoshughulikia uzoaji wa
taka ambao wamekuwa
wakilalamikiwa na wananchi.
Kwa upande
wao watendaji wa baadhi ya
taasisi wakiwemo Dr. Christopher Nzela kutoka chama
cha msalaba mwekundu
wamesema udhibiti wa ugonjwa wa
kipindupindu ni jambo linalowezekana tena
lisilo na gharama
kinachohitajika ni kila mmoja akitimiza
wajibu wake.
Iidadi ya wagonjwa
wa kipindupindu katika
mkoa wa arusha imekuwa
ikionhezeka na kupungua
na hadi sasa
wagon jwa watano wamelazwa
katika kituo cha afya
cha levolosi wakiendelea
na matibabu na
kutokana na kukithiri
kwa uchafu mkoa
wa arusha umetenga
siku ya jumamosi
ya mwisho wa
mwezi kuwa ni
ya kufanya usafi wa
jumla.
0 comments:
Post a Comment