Watu 36 tu katika kila watu 100 ya Watanzania, ambayo ni sawa na asilimia 36, ndiyo wanaopata huduma ya maji ya bomba nchini .
Wengine wengi hutegemea maji ya visima au maji ya kwenye madimbwi ambayo kwa ujumla siyo safi na salama na kwamba k atika suala la upatikanaji wa maji, tofauti kati ya wakazi wa mijini na vijijini ni kubw a.
Matokeo hayo yametolewa na taasisi ya TWAWEZA kwenye muhutasari wa utafiti wenye jina la Nusu Nusu yaliyotokana na m aoni ya wananchi kuhusu upatikanaji wa maji safi.
Muhutasari huu umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kwa njia ya simu za mikononi.
Licha ya kuanzishwa kwa Mpango wa Serikali wa Matokeo Makubwa Sasa na ku k a milika kwa kipindi cha Malengo ya Maendeleo ya Milenia,upatikanaji wa maji haujabadilika katika kipindi cha mwaka jana.
Matokeo yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,852 wa Tanzania Bara kati ya tarehe 9 Septemba na 26 Septemba mwaka huu na Zanzibar haikuhusishwa kwenye matokeo hay o .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment