Uganda ni nchi yenye viwango vikubwa mno vya rushwa. Waziri wa Mambo ya
Kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliangazia suala hilo wakati
alizuru nchini humo mwishoni mwa wiki katika ziara yake ya barani
Afrika
Ilichukua muda, lakini serikali ya Uganda na Gauff, kampuni ya kiwango
cha wastani yenye makao yake mjini Nuremberg, Ujerumani, wamesaini
makubaliano ya mkakati wa ujenzi wa bandari mpya ya Kampala katika eneo
la Bukasa. Kampuni hiyo imekuwa ikiutafuta mradi huo tangu mwaka wa
2008.
Muasisi wa kampuni hiyo Helmut Gauff alisema Wajerumani hawakubali
rushwa na Waganda wanafahamu hilo. Vinginevyo, mambo yangesonga haraka.
Labda ingechukua miaka miwili pekee badala ya mitatu kusaini kandarasi
hiyo.
Saini waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier inaipa
kandarasi hiyo kiwango fulani cha uzito. Nchini Uganda, kituo cha tatu
katika ziara yake ya Afrika, Steinmeier alisema mara si moja kuwa
Ujerumani ina matarajio fulani kutoka kwa washirika wake "Kupambana na
rushwa - katika nchi nyingi - ni suala ambalo ushiriki zaidi unaweza
kutarajiwa." Hata hivyo, nasisitiza kwamba "Mataifa ya Afrika Mashariki
ni kanda ambayo Ujerumani na Umoja wa Ulaya wanapaswa kutafuta
ushirikiano wa karibu".
Kwanza kabisa kabla ya yote, katika vita dhidi ya rushwa, katika nchi
nyingi ambazo tunazuru, kuna mengi ya kupendeza kuhusiana na hilo. Hili
sio suala la mawazo ya kutamani bali suala la utenda kazi na faida.
Uganda inaorodheshwa ya 142 kati ya 175 kwenye viwango vya nchi fisadi
ulimwengu na Shirika la Transparency International. Inasemekana kuwa
kila mradi wa miundo mbinu unaoidhinishwa nchini humo kwanza lazima
upitie dawati la Rais Yoweri Museveni. Ni yeye anayeamua ni nani anapata
mradi huo. Gauff amesema hilo sio kweli – lakini pia akasema mtoto wake
wa kiume ana mawasiliano mazuri na rais Museveni. Mbali na hayo,
alisema kampuni yake huwekeza katika miradi ya kijamii kama vile taasisi
za elimu na makazi ya mayatima.
Bandari ya Kampala katika eneo la Bukasa ina nafasi kubwa ya kujengwa
kwa sababu kuna mahitaji ya kweli. Bila hiyo, Uganda ambayo haina njia
ya moja kwa moja ya baharini, inaweza tu kuuza nje bidhaa zake kwa
kutumia barabara ya Ukanda wa Kaskazini uliojazana kupita kiasi kuelekea
bandari ya Mombasa, Kenya.
Bukasa itakuwa chanzo cha barabara mpya ya Ukanda wa Katikati inayofika
katika bandari za nchi jirani Tanzania. Huenda ikasababisha mabadiliko
makubwa ya kiuchumi katika eneo hilo zima. Huenda – ikiwa rushwa
haitabakia kuwa mfano imara kabisa wa kibiashara.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment