Image
Image

Bamia inauwezo wa kutibu magonjwa mengi kiafya.

Bamia ni miongoni mwa mboga mboga ambazo tunaweza kuziweka kwenye kundi la mboga za majani, lakini mboga hii nayo inasifika sana kwa kuwa na virutubisho muhimu vya kutosha
Kwanza taarifa ikufikie kwamba bamia ni moja ya chanzo kizuri cha nyunyuzi yaani 'fiber' ambapo husaidia sana kurahisisha umeng'enyaji wa chakula tumboni.
Lakini pia bamia nayo husaidia sana kurekebisha sukari  mwilini na kumue[usha mhusika kuwa katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya moyo.
Aidha, bamia zinakitu kiitwacho 'antioxidants' ni kirutubisho ambacho husaidia kupambana na magonjwa ya moyo pamoja na saratani pia.

Ndani ya bamia kuna aina mbalimbali za madini pamoja na vitamin ikiwa ni pamoja na vitamin A, B, C na K, huku madini ikiwa ni pamoja na copper, magnesium, potassium na manganes 
Uwepo wa vitamin C unaifanya mboga hiyo kuwa na uwezo wa kurutubisha afya ya ngozi kutokana na kuwa na uwezo wa kurejesha tishu za ngozi zilizokufa.
Halikadhalika bamia pia ni suluhisho la matatizo ya pumu mboga hii husaidia kupunguza athari za matatizo hayo pamoja na dalili zake kwa ujumla.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment