Benki ya dunia imesema inaridhishwa na utendaji kazi wa
serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dr.John Pombe Magufuli na kwamba
inaunga mkono jitihada zake za kubana matumizi,kuongeza mapato na kuhakikisha
huduma za kijamii zinawafikia watanzania wote na kwamba iko tayari kushirikiana
na tanzania katika miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na upanuzi wa bandari ya
dar es salaam,ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kimataifa.
Hayo yamebainika katika kikao kilichomkutanisha rais Dr.John
Pombe Magufuli na mwakilishi mkazi wa benki ya dunia Bi.Bella Bird ikulu jijini
dar es salaam ambapo katibu mkuu wa wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile
amesema benki hiyo inaridhishwa na utendaji kazi rais Dr.Magufuli na kwamba iko
tayari kushirikiana na Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni
pamoja na upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam.
Dr.Likwelile ameendelea kufafanua maeneo ambayo yamegusiwa
katika mazungumzo baina ya rais Dr.Magufuli na mwakilishi huyo mkazi wa benki
ya dunia Bi.Bella Bird.
Takribani miradi zaidi ya ishirini na tisa imefadhiliwa na
benki hiyo ya dunia nchini ambapo kiasi cha dola bilioni nne zimekwishatolewa
na benki hiyo hapa nchini.
Endelea kufuatilia Taarifa zetu kufahamu zaidi,Like Page
yetu uwe wakwanza kupata habari.
0 comments:
Post a Comment