Image
Image

Diendere ameshtakiwa kwa kuhusika katika mauaji ya rais Sankara.

Kiongozi wa mapinduzi yaliyodumu kwa muda mfupi nchini Burkina Faso Jenerali Gilbert Diendere ameshtakiwa kwa kuhusika katika mauaji ya rais wa zamani wa nchi hiyo Thomas Sankara alieuawa mwaka 1987.
Jenerali Gilbert Diendere ni afisa wa ngazi ya juu zaidi kushatakiwa kwa mauaji hayo.
Rais Sankara aliuawa na kundi la askari, lakini mazingira halisi ya kifo chake yamesalia kutojulikana.
Bwana Sankara aliyekuwa na itikadi kali za mrengo wa kushoto anaelezewa kama " Che Guevara wa Afrika", na amesalia kuwa shujaa kwa waafrika wengi.
Baada ya kifo chake Blaise Compaore alikua mrithi wake akisalia madarakani kwa miaka 27.
Jenerali Diendere, ambaye aliendelea na kuwa mkuu wa ujasusi katika utawala wa Compaore, aliangaliwa kama rafiki wa karibu namshirika mkuu wa kisiasa wa bwana Sankara wakati wa kifo chake.
Wakati wa utawala wa Compaore uchunguzi uliofanyika kuhusiana na mauaji hayo ulikuwa wa mafanikio kidogo.
Serikali ya mpito, iliyochukua mamlaka baada ya kung'olewa madarakani kwa Compaore mwaka 2014, iliahidi kuchunguza mauji hayo upya.
Maafisa wengine 10 wameshtakiwa hadi sasa kuhusiana na mauaji ya Sankara.
Jenerali Diendere tayari yuko mahabusu, akikabiliwa na mashtaka kuhusiana na mapinduzi ya siku saba ya mwezi wa Septemba.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment