Image
Image

Lates News:Kimenukaa Bandari Maofisa 8 nje mwinjaka wa uchukuzi afutwa kazi.

Rais DR. JOHN POMBE MAGUFULI ametengue uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania Bwana AWADHI MASAWE na Mwenyekiti wa Bodi ya Bandari Profesa JOSEPH MSAMBICHAKA na  kuvunja  bodi yake.
Uamuzi huo umetangazwa jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Bwana KASSIM M. MAJALIWA wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema Rais pia amewasimamisha maafisa wanane wasimamizi wa bandari kavu waliohusika na kutoa makontena kwenda kwa wateja bila kulipiwa ushuru na maafisa wengine wanne ambao walihusika kutoa makontena hayo kutoka bandarini kwenda bandari kavu bila kulipiwa ushuru.
Waziri Mkuu ameongeza kuwa rais pia ameagiza wote hao waliohusika wawekwe chini ya ulinzi kusaidia polisi katika uchunguzi wao ili kurejesha fedha zilizopotea kutokana na kupotea kwa makontena hayo.
Aidha Rais MAGUFULI ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi DR. SHABAN MWANJAKA kutokana na dosari alizobaini Waziri Mkuu wakati wa ziara yake kwenye karaka ya Kampuni ya Reli Tanzania TRL.
Wakati huo huo  amhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imewapatia mafunzo  maafisa wake wa forodha hapa nchini kusimamia wafanyabiashara wao ipasavyo ili kuhakikisha wanalipa kodi inayostahiki kwenye bandari ya Dar es Salaam.
Hiyo inafuatia agizo la Rais DKT JOHN MAGUFULI kuwataka wafanyabiashara wote wanaopitishia mizigo katika bandari ya Dar es salaam kulipa kodi ainayotakiwa.
Kwa upande wao maafisa hao wa foprodha wa Kongo wamesema hawatakuwa tayari kuona wafanyabiashara wao wakipitisha kinyemela mizingo bandarini hapo bila kulipa ushuru na kwamba watahakikisha hakuna udanganyifu wowote utakaofanywa na wafanyabiashara wao.
Kwa upande wake Afisa Mwakilishi wa Kodi nchini Kongo Bwana  PETER MOLLISHO amesema serikali ya Kongo inaunga mmkono juhudiza Tanzania za kudhibiti wakwepa kodi na kwamba watajitahidi kuendelea kutoa elimu wafanyabiashara wa Kongo.
Akizungumza kwa niaba ya wafanyabiashara wa Kongo waliko Tanzania, Mwenyekiti wa wafanyabiasahra hao Bwana  MKENDA KABOBO, amesema wanaunga mkono kauli ya rais wa Tanzania na kuahidi kutokufumbia macho wafanyabiashara wanaokwepa kodi.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment