Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaendelea Le Bourget . Mawaziri wa
mataifa 195 wanalazimika kusawazisha misimamo ya nchi za kusini na
zile,za kaskazini,wakitaka kufikia makubaliano ijumaa, kama
ilivyopangwa.
Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaendelea Le Bourget ,karibu na
Paris. Mawaziri wa mataifa 195 wanalazimika kusawazisha misimamo ya nchi
za kusini na zile,za kaskazini,wakitaka kufikia makubaliano kesho
ijumaa, kama ilivyopangwa.
Pindi wakikubaliana hayo yatakuwa makubaliano ya kimataifa yatakayozuwia
majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, yanayoshuhudiwa
kila kukicha.
Zikiwa zimesalia chini ya saa 36 kabla ya muda uliowekwa
kukamilika,mkutano huo wa Le Bourget unaonyesha unazorota katika masuala
matatu muhimu-na majadiliano ya jana usiku yamebainisha njia ya kufikia
makubaliano imejaa vizingiti.
Fabius awapa moyo wajumbe mkutanoni.
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Laurent Fabius,ambae ndie
mwenyekiti wa mkutano huo unaojulikana kama COP21,aliwakabidhi wajumbe
196 mswaada wa waraka,uliofupishwa na ambao takriban nusu ya vifungu
vyake vinaonyesha viko tayari kuratibiwa."Ni waraka mfupi wa kurasa 29
badala ya 43,ukijumuishwa mswaada wa makubaliano na uamuzi uliopitishwa
na COP21. Na kulinganisha na waraka wa awali,vifungu ambavyo vinasubiri
ufafanuzi vimepungua kwa kadiri asili mia 75. Kwa hivyo kishindo
kimepungua sana,ingawa bado ni kikubwa."Amesma Fabius.
Miongoni mwa mada zinazobidi kupatiwa ufumbuzi ni pamoja na jinsi ya
kugharimiwa miradi ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi baada ya
mwaka 2020,na vipi kutekeleza mwongozo "kuhusu jukumu la pamoja lakini
kwa viwango tofauti."
Kabla ya duru ya mazungumzo jana usiku,wawakilishi wa nchi hizo
zinazoinukia walielezea msimamo wao wakipinga kuwekwa mstari mmoja na
nchi za kaskazini,wanazosema zinabeba jukumu la jadi la kuongezeka hali
ya joto duniani na ambazo wanasema zenye uwezo mkubwa zaidi wa
kukabiliana na majanga kama hayo.
Waraka unakosolewa na wawakilishi wa nchi zinazoinukia.
"Makubaliano ya kudumu hayawezi kupatikana kwa kufifiisha jukumu la
kihistoria na kwa kuwatumbukiza ndani ya chungu kimoja wachafuzi na
wahanga wa uchaguzi-"Amesema Prakash Javadekar-waziri wa mazingira wa
India ambae nchi yake inashikilia nafasi ya mbele katika mazungumzo ya
Le Bourget.
Akiwakabidhi mswaada wa makubaliano waziri wa mambo ya nchi za nje wa
Ufaransa Laurent Fabius aliwahimiza wajumbe mkutanoni waridhiane kuhusu
mswaada mpya hadi ifikapo leo jioni.Makubaliano kamili yanatarajiwa
kesho jioni.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment