Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 baada ya kufanya naye mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene kayihura Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 na kufanya naye mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Rwanda hapa Nchini Mhe. Eugene kayihura Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 baada ya kufanya naye mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipokutana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero Ikulu jijini Dar es salaam Desemba 21,2015 na kufanya naye mazungumzo.
Katika tukio jingine rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amemuhakikishia mwakilishi mkazi
wa benki ya maendeleo ya Afrika AFDB Dkt.Tonia Kandiero kuwa serikali yake ya
awamu ya tano itaendelea kushirikiana na benki hiyo katika utekekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo.
pamoja na kumhakikishia ushirikiano rais Magufuli
ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji
wa miradi na badala yake ameshauri uwepo utaratibu wa haraka unawezesha kuanza
kwa miradi katika kipindi kifupi baada ya fedha kutolewa huku Dkt.Tonia
Kandiero akimpongeza rais Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kuwa rais wa
jamhuri ya muungano wa tanzania katika awamu ya tano,amemhakikishia kuwa benki
ya AFDB iko tayari Kuendelea kushirikiana na tanzania katika maendeleo kama
amabavyo imekuwa ikifanya na kwamba kwa sasa imetenga dola bilioni mbili nukta
tatu kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.
Pia katika hatua nyingine rais wa jamhuri ya Tanzania
Dkt.John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Rwanda
hapa nchini Mh.Eugene Kayihura Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Balozi kayihura amesema rais kagame amefurahishwa na
hatua ambazo rais Magufuli anazichukua hasa katika usimamizi na utendaji kazi
wa bandari na kumhakikishia kuwa Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania
hasa kuitumia bandari ya Dar es Salaam ambayo hupitisha asilimia zaidi ya 70 ya
mizigo ya Rwanda.
0 comments:
Post a Comment