Mchezaji nyota wa tenisi kutoka Uingereza Johanna
Konta amemshinda Venus Williams 6-4 6-2 na kufika raundi ya pili ya shindano la
tenisi la Australian Open mjini Melbourne.
Konta, 24, alipata ushindi kwa kutumia dakika 79
huku bingwa wa Grand Slam Williams, ambaye alikuwa amefungwa bendeji paja lake
la kushoto, akionekana kutatizika.
“Droo ilipofanywa na nikaona nilikuwa nimepangwa
kucheza na nani, niliomba tu niweze kudumu uwanjani zadi ya saa moja,” amesema
Konta.
Andy Murray pia alishinda lakini Dan Evans
akabanduliwa.
Aljaz Bedene atacheza baadaye.
Konta, aliyefika hatua ya 16 bora katika US Open mwaka
2015, sasa atakutana na mshindi kati ya Carina Witthoeft na Saisai Zheng,
katika raundi ya pili.
Konta aliyeorodheshwa nambari 47 duniani, alikuwa
akicheza mara ya kwanza katika Australian Open na ndiye mwanamke Mwingereza
pekee aliyesalia katika droo ya mashindano ya mchezaji mmoja mmoja baada ya
Heather Watson kushindwa Jumatatu.
0 comments:
Post a Comment