Polisi nchini Kenya wamenasa noti bandia za jumla ya
$693m (£485m) baada ya kufanya msako katika nyumba moja jijini Nairobi.
Watu wawili, mmoja kutoka Cameroon na mwingine
kutoka Niger, wamekamatwa kuhusiana na pesa hizo.
Mkuu wa polisi Joseph Boinett akitangaza kupatikana
kwa pesa hizo, amewaambia wanahabri kwamba hicho ni “kiasi kikubwa sana” cha
pesa.
Amesema noti bandia za euro 369 milioni pia
zimepatikana, pamoja na mitambo ya kutengeneza noti bandia.
Polisi walifanya msako baada ya kupokea habari za
mfanyabiashara aliyetapeliwa Sh40 milioni za Kenya baada ya kuhadaiwa kwamba
zingeongezwa mara tatu na kuwa Sh120 milioni.
Kwa jumla, pesa hizo zilizopatikana katika mtaa wa
South C, zikibadilishwa na kuwa shilingi za Kenya zinafikia Sh110 bilioni
ambazo ni sawa na shilingi trilioni 2.3 za Tanzania.
0 comments:
Post a Comment