Kenya bado iko katika hali ya sintofahamu baada ya
shambulio lililosababisha vifo vya wanajeshi kadhaa katika kambi ya jeshi la
Kenya nchini Somalia Ijumaa, Januari 15, wanajeshi wengi wanashukiwa kuwa bado
wanashikiliwa na wapiganaji wa kundi la Al-Shebab.
Wanajeshi wengine wanashukiwa kuwa wamejificha
katika maeneo jirani,wakati ambapo operesheni ya kuwaokoa imeanzishwa na jeshi
la Kenya.
Wakati huo huo,askari waliojeruhiwa na wale
walionusurika wamerejeshwa katika makundi madogo mjini Nairobi.
Habari hii imegonga vichwa vya habari kwenye
magazeti ya Nairobi, ambapo, manusura wameonekana kwenye picha wakishuka ndege.
Jumatatu, Januari 18, askari 16 waliojeruhiwa, wakiwa hawana furaha yoyote,
wamewasili nchini Kenya. Inaarifiwa kuwa askari hao waliokolewa katika kichaka
nchini Somalia karibu na kambi ya El Adde siku mbili baada ya shambulizi hilo.
Upande wa jeshi, inaonekana kuwa shambulizi hilo ni
pigo kubwa kwao. Mkuu wa majeshi ya Kenya, Mwathethe Samson, amefanya mkutano
na waandishi wa habari Jumatatu hii.
"Tumeanzisha operesheni ya kuwaokoa askari
wetu. Tutapambana nao kwa kina hadi katika maeneo wanakojificha, na tutaendelea
hadi mwisho, kwa heshima ya kila tone la damu linalomwagika kutoka kwa ndugu
zetu", Samson Mwathethe amesema.
Hakuna idadi yoyote ya askari waliouawa, kujeruhiwa
au kutekwa nyara ambayo imetolewa na jeshi la Kenya, ambalo si kawaida yake ya
kutoa taarifa zinazohusiana na hasara linalopata nchini Somalia. Kwa upande
wake, kundi la Al-Shebab ambalo lina tabia ya kuongeza chumvi katika matokeo ya
shughuli zake. Kundi hili limesema kuwa limewaua askari 121wa Kenya katika
shambulio hilo.
Serikali ya Kenya kupitia Katibu Dola anayehusika na
maswala ya Ulinzi Rachael Omamo, imewataka raia kuwa watulivu kufuatia tukio
hilo. "Tunapaswa kudumisha umoja wetu. Tafadhali, tusitofautiane kutokana
na hali hii, muwe na subira.Taarifa itatolewa mara moja ikithibitishwa.Tuko
tayari kuwarejesha askari wetu nyumbani", amesema Rachael Omamo.
Kwa mujibu wa vyanzo nchini Somalia, mapigano makali
bado yanaendelea katika jimbo la El Adde. Ndege za jeshi la Kenya zimeingia
Somalia zikisaidiwa na askari wa nchi kavu katika jitihada za kurejesha eneo
hilo, kuwaokoa wale walio mafichoni na wale ambao walikamatwa.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment