Vyanzo
vya kiintelijensia nchini Uingereza vimeiambia BBC kwamba vinaamini wamemtambua
mwanaume mwenye asili ya nchi hiyo ambaye anaonekana katika mkanda wa video wa
hivi karibuni wenye kupigia chapuo propaganda za kundi la kigaidi la wanamgambo
wa Islamic State.
Vyanzo
hivyo vimemtaja mtu huyo kuwa ni Siddhartha Dhar, ambaye anaaminika alikuwa
akiishi Mashariki mwa London.
Kwa
asili Siddhartha anatajwa kuwa ni Mhindi ambaye aliamua kubadilisha dini yake
ya awali na kuwa Mwislamu na inafahamika kuwa baada ya hapo aliamua kuijiunga
na kundi lenye msimamo mkali la Al Muhajiroun.
Msemaji
wa kundi hilo ameiambia BBC kuwa sauti inayosikika katika mkanda huo wa video
haijakosewa asilani, hata hivyo dadake na Siddhartha Dhar amenukuliwa akisema
kwamba hana uhakika kwamba sauti hiyo ni ya kaka yake.
Ikumbukwe
kwamba mkanda huo wa video unaonesha mauaji ya wanaume watano ambao
wanashutumiwa kwa kosa la kuichunguza kwa siri Uingereza.
0 comments:
Post a Comment