Ligi Kuu Bara imesimama wiki mbili kupisha michuano
ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Zanzibar hivi sasa.
Ingawa michuano hii haitambuliki kimataifa, lakini
imekuwa ikizishirikisha pia timu kutoka nje ya nchi.
Kwa mfano, mwaka huu michuano hiyo inazishirikisha
timu 12, kati ya hizo imealikwa moja kutoka nchini Uganda, URA. Inaunga na timu
nyingine za Bara na visiwani kucheza michuano hiyo ya wiki mbili.
Tambarare Halisi tunaamini kwamba Kombe la lina
nafasi kubwa ya kuziandaa timu za Tanzania zinazotarajia kushiriki michuano ya
kimataifa kuanzia mwezi ujao.
Yanga, miongoni mwa timu kutoka Bara zinazoshiriki
michuano hiyo Zanzibar, mwaka huu itaiwakilisha nchi kwenye michuano ya Klabu
Bingwa na Azam FC kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kwa kuzingatia umuhimu wa mashindano hayo, tunaamini
Azam, ambayo nayo inashiriki Kombe la Mapinduzi kama ilivyo Yanga, zote kwa
pamoja zitayachukulia mashindano haya kama sehemu ya kujitengeneza.
Yanga imeamua kwenda wachezaji wake wote ili kuwapa
nafasi ya kucheza, kadhalika wawakilishi wenzao Azam FC.
Lakini pia michuano hiyo ni fursa ya kujiimarisha
zaidi kwa timu zote, ikiwamo Simba na Mtibwa Sugar kabla ya kurejea kwenye
mechi za ligi kuu.
Tunaamini timu zote zitatumia nafasi hiyo vizuri
ikiwa ni pamoja na kuyafanyia kazi makosa na udhaifu utaoonekana wakati wote wa
mashindano.
Zana kwamba mashindano hayo hayana taswira ya
kimataifa, isizifanya timu kucheza katika hali ya kujifurahisha, badala yake
zicheze kwa ushindani wa kweli.
Tungependa kuzikumbusha timu zote zinazoshiriki
Kombe la Mapinduzi kuwa, timu zinazotumia muda wake vizuri kujiandaa na
mashindano mbalimbali, ndizo zinazokuwa jirani na mafaniki kuliko zile ambazo
hazina utamaduni huo.
Hivyo, viongozi wala wachezaji wasiwe na sababu
zozote za kubeza mashindano hayo na kuona kama sehemu ya kupoteza muda.
Pia Nipashe tungependa kuchukua nafasi hii
kuwapongeza waandaaji wa Kombe la Mapinduzi, Chama cha Soka Zanzibar (ZFA),
ambao wamesema wameboresha kwa kiasi kikubwa michuano ya mwaka huu.
Katibu Msaidizi wa ZFA, Masoud Attai alisema dhamira
yao mwaka huu ni kuhakikisha mashindano hayo yanabeba sura ya ushindani zaidi
kuliko wakati uliopita.
Katika hilo, wameamua kuzipa nafasi zaidi timu za
Tanzania kwa kupunguza idadi ya timu alikwa.
Sababu kuwa ni kuhakikisha michuano hiyo
inayofanyika nyumbani iwe na faida kubwa kwa wenyeji.
Zawadi ya Sh. milioni 10 kwa mshindi wa kwanza na
Sh. milioni 5 kwa mshindi wa pili zitakuwa kiini cha ushindani wa kweli
miongoni mwa timu shiriki.
0 comments:
Post a Comment