Kiongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam
nchini Sheikh Ponda Issa Ponda amepinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar
(ZEC) kurudia uchaguzi visiwani humo.
Amedai kitendo cha ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi
uliofanyika Octoba 25 mwaka 2015, hakikuwa na sababu za msingi kutokana na
uchaguzi huo kufanyika kwa mujibu wa sharia na kanuni za katiba ya Zanzibar.
Ikiwa ni siku moja baada ya Baraza Kuu la Waislamu
Tanzania (BAKWATA) kuunga mkono Tume ya Uchaguzi Zanzibar kuhusu kurudiwa kwa
Uchaguzi Machi 20, Mwaka huu, Sheikh Ponda amesema kurudia kwa uchaguzi huo si
njia sahihi ya kumaliza mgogoro huo.
Amesema Uchaguzi uliofanyika Oktoba 25 mwaka 2015
ulikuwa halali kutokana na taarifa za waangalizi wa ndani na nje ya nchi.
Sheikh Ponda ameungana na viongozi wa Chama cha CUF
waliopinga kushiriki marudio ya uchaguzi huo, wakidai Mwenyekiti wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wa kufuta matokeo ya uchaguzi huo ni batili kutokana na
kasoro nyingi za kikatiba na sheria.
Kwa Mujibu wa Ponda amemwomba Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo kama alivyoahidi bungeni.
Mwenyekiti wa ZEC, Salim Jecha, alifuta matokeo ya
uchaguzi wa Oktoba 25, 2015 kwa madai kuwa kuna Masanduku ya kupigia kura
hayakupewa ulinzi wa kutosha huku baadhi ya maajenti wa vyama pamoja na maafisa
wa uchaguzi wakidaiwa kufukuzwa katika vituo kadhaa.
Sababu nyingine zilizotolewa zilikuwa ni kuwepo kwa
madai ya Vijana kuvamia vituo vya kupigia kura wakiwa na lengo la kuzua ghasia,
na Vyama vya kisiasa kuingilia tume hiyo na kura kuharibiwa hususan zile
kutoka Pemba..
Hata hivyo, licha ya mvutano wa hapa na pale, baadhi
ya vyama vya siasa vimekubali kushiriki marudio ya uchaguzi huo, huku wananchi
wa Zanzibar wakiombwa kuunga mkono uamuzi huo kwa kujitokeza kwa wingi siku
hiyo.
0 comments:
Post a Comment