Virusi hai vya Zika vyapatikana katika mate na
mikojo ya wagonjwa,wanasayansi wa Brazil wamesema.
Matokeo hayo hayamaanishi kwamba ugonjwa huo unaweza
kusambazwa kupitia maji maji hayo ya mwilini.Sababu kuu ya kuenea kwa virusi
hivyo ni kupitia kuumwa na mbu,lakini wanasayansi wanachunguza njia nyengine.
Huku maambukizi ya Zika yakiwa sio makali,ugonjwa
huo umehusishwa na maelfu ya watoto waliozaliwa na kasoro.
Virusi vya Zika pia vimepatikana katika majimaji
mengine ya mwilini katika mripuko mwengine uliotokea eneo la Polynesia,lakini
mamlaka ya Brazil inasema kuwa hii ni mara ya kwanza virusi hai vya Zika
kupatikana.
Paula Gadelha,mkuu wa taasisi ya Fiocruz ambayo
inashirikiana na wizara ya Afya amesema:''Virusi hivyo vya Zika vimepatikana
katika Mate na mikojo''.
Wanasaynsi wa Brazil
''Lakini hiyo hainamishi kwamba kuna uwezekano wa
kuenea kwa virusi hivyo kupitia mate na mikojo.Hatari ya kuenezwa kwa virusi
hivyo kupitia maji maji ya mwilini uliangaziwa nchini Marekani ambapo kituo cha
udhibiti wa magonjwa kinaamini kisa kimoja kilisambazwa kupitia ngono''.
Hatahivyo kumekuwa na kesi mbili pekee za usambazaji
wa virusi hivyo kupitia ngono.
0 comments:
Post a Comment