Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es salaam
umezidi kuchukua vichwa vya habari baada ya kuahirishwa mara kadhaa na hata
mara ya mwisho kuibuka kwa vurugu ambazo zilipelekea baadhi ya Wabunge wa Chadema na Madiwani wake
kufikishwa mahakamani na baadae kuachiliwa kwa dhamana.
March 10 2016 Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), Saed
Kubenea amehitajika polisi kwa tuhuma za kuhusika na vurugu wakati
uchaguzi huo ulipoahirishwa February 27 2016. Saed Kubenea
ameelezea kuhusiana na wito huo wa polisi kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo na
amesimulia ilivyokuwa….
’Nimefuatwa na askari kama sita wakiniambia kwamba
niko chini ya ulinzi ninahitajika makao makuu ya polisi Dar es salam nikahoji
kosa langu ni nini? wakasema nikajibu tuhuma juu ya vurugu zilizotokea
katika uchaguzi wa Meya wa Dar es salaam‘:-Saed Kubenea
Pia ameeleza kwamba hapo awali wakati tukio
linatokea yeye hakuwa kwenye orodha ya washitakiwa kwa hiyo anakwenda
kuwasikiliza na kama atapelekwa mahakamani anaamini haki itatendeka, Kubenea
ameeleza..
’ninachokumbuka mimi nilifika makao makuu polisi
kuwasilisha malalamiko juu ya amri iliyotolewa kwamba uchaguzi ule uzuiliwe,
niliwathibitishia polisi kwamba amri ile ilikuwa haramu na ilikuwa imeexipire
kwa hiyo ni lazima wachukue hatua za kisheria dhidi ya wahusika, na SP
Ndalama ambaye ni mkuu wa upelelezi wa mkoa wa kipolisi Ilala alikuwepo
na alinipa orodha ya watu wanaotakiwa mimi jina langu halikuwemo‘:-Saed Kubenea


0 comments:
Post a Comment