Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli amewathibitisha watendaji wakuu wa taasisi mbili za serikali.
Waliothibitishwa ni Bw. Alphayo Kidata, aliyekuwa
Kaimu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ambaye anakuwa
Kamishna Mkuu wa TRA, na Bw. Valentino Mlowola aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ambaye anakuwa
Mkurugenzi Mkuu wa (TAKUKURU).
Watendaji hawa wamethibitishwa kuanzia leo tarehe 13
Machi, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam
13 Machi, 2016


0 comments:
Post a Comment