Rais wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli
amemsimimisha kazi Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam Bwana.Willison Kabwe na
kuagiza uchunguzi ufanyike mara moja kuanzia sasa.
Kusimamishwa kazi kwa bwana Kabwe nikutokana na
tuhuma zinazomkabili za kuhusika katika kashfa ya kusaini mikataba mbalimbali
ambayo imedaiwa kuwa na utata baada ya muda wake kuisha ikiwemo utaratibu wa
upangaji wa jengo la Machinga Compex, utoaji wa tozo katika kituo kikuu cha
mabasi ubungo pamoja na ukusanyaji wa kodi za Maengesho ya Magari katika ya
jiji la Dar es Salaam.
Rais Daktari Magufuli ametoa agizo hilo wakati
akizindua daraja la Kigamboni ambalo sasa linaitwa daraja la Nyerere ambapo
ujenzi wake umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 254 hadi kukamilika kwake na
kuagiza watembea kwa miguu kuvuka bure katika daraja hilo huku vyombo
mbalimbali vya usafiri vikitakiwa kulipa fedha ambayo itapangwa na wizara ya
ujenzi uchukuzi na mawasiliano.
0 comments:
Post a Comment