Wananchi wa chad
leo wanapiga kura kumchagua rais wa nchi hiyo na mwelekeo unaonesha
kuwa, rais wa sasa Idriss Deby,anapewa nafasi kubwa ya kurejea madarakani.
Rais Deby,ambaye aliingia madarakani kwenye
mapinduzi ya kijeshi miaka 26 iliyopita, anakabiliwa na ushindani kutoka kwa
wagombea 12, lakini anatarajiwa kushinda kwa awamu nyingine.
Katika wiki za hivi karibuni maandamano yalipigwa marufuku na baadhi ya wapinzani wa serikali kukamatwa.
Alhamisi
iliyopita polisi walilazimika
kutumia risasi za moto na mabomu ya
machozi kuwatawanya mamia ya
waandamanaji baada ya waendesha mashitaka kutaka wanaharakati watano wanaoipinga serikali
wafungwe jela miezi sita.
Mwaka 2011 wapinzani walisusia uchaguzi mkuu.
0 comments:
Post a Comment