Image
Image

Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kufungiwa kwa kushindwa kukidhi vigezo vya usafi.


Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa imenusurika kufungwa kutokana na kushindwa kukidhi vigezo vya usafi vya baraza la taifa la usimamizi wa mazingira (NEMC) baada ya kichoma taka chake kuharibika na kushindwa kufanya kazi kwa kipindi cha miezi minne ambapo serikali imeuagiza uongozi wa mkoa na hospitali kufanya matengenezo ya kichoma taka hicho haraka.

Hiki ni kichoma taka kilicho haribika katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na mazingira Luhaga Mpina ametoa agizo hilo hospitalini hapo na kutoa muda wa mwezi mmoja kwa uongozi wa mkoa na hospitali hiyo kutekeleza agizo lake ambapo amesema amelazimika kutoa agizo hilo kutokana na ummuhimu wa huduma zitolewazo hospitalini hapo lakini ukosefu wa kichoma taka hicho kisheria unamlazimu kufunga hospitali hadi kitakapoanza kufanya kazi.

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano na mazingira Luhaga Mpina.
Kwa upande wake mratibu wa baraza la taifa la usimamizi wa Mazingira nchini Kanda ya nyanda za juu Kusini Godlove Mwansojo ameshauri taka zinazozalishwa hospitalini hapo zitenganishwe ili taka ngumu zisizooza zihifadhiwe hadi hapo kichoma taka hicho kitakapotengemaa na kufanya kazi.
Akiwa hospitalini hapo Naibu Waziri Luhaga Mpina ameelezwa kuhusu ukosefu wa eneo la kupanua hospitali hiyo kutokana na kubanwa na gereza la mkoa wa Iringa ambapo ameutaka uongozi wa mkoa kupeleka mapendekezo serikalini ya kuomba kuhamishwa kwa gereza hilo ili eneo hilo libakie kwaajili ya hospitali hiyo pekee.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment