HASSAN Hanafi, mwanahabari aliyesaidia kundi la
Al-Shabaab kuua wanahabari wenzake nchini Somalia ameuawa.
Shirika la Habari la Uingereza (BBC) limeripoti
kuwa, Hanafi ameuawa kwa kupigwa risasi mapema leo baada ya kuhukumiwa kifo na
mahakama ya kijeshi nchini humo.
Hanafi alipatikana na hatia ya kushiriki katika
mauaji ya Sheikh Noor Mohamed Abkey (mhariri wa Shirika la Habari la SONNA),
Sa’id Tahlil Warsame, (Mkurugenzi wa HornAfrik, Mukhtar Mohamed Hirabe,
Mkurugenzi wa Radio Shabelle na wanahabari wengine.
Alikamatwa nchini Kenya Agosti mwaka 2014 na
kupelekwa Somalia mwishoni mwa mwaka jana. Ambapo alihukumiwa kifo na Mahakama
ya kijeshi ya ngazi ya chini ya nchini Somalia tarehe 3 Machi mwaka huu.
Kwa mujibu wa shirika hilo, mwanahabari huyo alikiri
kuhusika na mauaji ya wanahabari watano.
Hanafi ambaye ni mwanachama wa kundi la al-Shabab
alikamatwa nchini humo Agosti mwaka jana akiwa kwenye harakati za kutoroka.
Upande wa mashtaka ulimshtumu kwa kuhusika na mauaji
ya waandishi wengine maarufu nchini Somalia mwaka 2007.
Hanafi alijiunga na wapiganaji wa kundi la al-Shabab
miaka michache iliopita baada ya kufanya kazi na Redio Andalus ambayo ndio
inayotoa taarifa za kundi hilo.
Abdinoor Aden, Mwandishi wa BBC anasema Hanifa
alikuwa maarufu kwa wasikilizaji wengi wa redio nchini Somalia baada ya
kujiunga na idhaa maarufu ya Quran FM. Aliondoka mwaka 2006 na kujiunga na
mtandao huo.
0 comments:
Post a Comment