Nchi zipatazo 175
zimetia saini kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mkataba wa Paris wa
Mabadiliko ya Tabianchi ikiwa ni rekodi ya idadi kubwa ya nchi kutia saini
mkataba huo mpya wa kimataifa.
Awali mataifa madogo yapatao 15 mengi yakiwa ya visiwa
vidogo yalikuwa yameridhia mkataba huo lakini nchi nyingine kadhaa zilitakiwa
kuchukua hatua hiyo ya pili kabla ya mkataba huo kunza kutumika.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema Mkataba wa Paris
utatengeneza maisha vizazi vyote vijavyo katika njia ya aina yake kwa hatma
iliyopo mikononi mwao.
Akizungumza mwanzoni mwa sherehe hiyo alisema sayari hivi
sasa ilikuwa inashuhudia rekodi ya joto duniani na muda ulikuwa unakwenda
kupambana na hali hiyo.
0 comments:
Post a Comment