Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
ALIYEKUWA
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh,
amefichua siri ya Rais Dk. John Magufuli kutumbua majipu kwa kasi, tangu
ameingia madarakani mwaka jana.
Akizungumza wakati wa kuzindua
ripoti mbili za Mpango wa Uhamasishaji Uwazi katika Mapato ya Madini,
Gesi na Mafuta (TEITI), mjini Dar es Salaam jana, Utouh alisema akiwa
CAG aliandaa ripoti nyingi ambazo utawala uliopita haukizifanyia kazi.
Alisema Rais Magufuli anatumia ripoti hizo kutumbua vigogo mbalimbali, kwa sababu amekuta mambo yako mezani.
“Ripoti zangu nikiwa CAG ndizo zinasomwa bungeni, zimeonyesha udhaifu maeneo mbalimbali ya taasisi za Serikali na nyingine.
“Nyingi
zilikabidhiwa zamani,viongozi waliopita hawakuzifanyia kazi…nawaambua
utumbuaji majipu unaofanywa na Rais Magufuli, utasaidia kuongeza kasi
ya ukusanyaji mapato na nidhamu sehemu za kazi.
Alisema ni jukumu la kila mwananchi kulinda rasilimali zilizopo na kwa kufanya hivyo, mapato yataongezeka.
Kuhusu
sheria ya madini iliyopitishwa mwaka jana, inayozungumzia uwazi na
uwajibikaji katika sekta ya madini, Utouh alisema imesaidia kuleta
nidhamu katika sekta hiyo, kwa sababu kabla ya hapo mapato mengi
yalikuwa yakipotea.
Naye Mwenyekiti wa TEITI, Jaji Mark Bomani
alisema taarifa za kazi za TEITI katika ripoti ya mwaka 2013/14,
zimesaidia kunufaisha uhamasishaji uwazi katika sekta ya madini nchini.
Alisema
sekta hiyo ilianza kushamiri mwaka 1990, haikuwa na manufaa kwa uchumi
wa nchi kwa vile mapato kwa Serikali hayakuwa wazi.
Alisema mwaka
2007, Rais mstaafu, Jakaya Kikwete aliunda kamati ya kuchunguza sekta ya
madini ambayo kwa miaka mingi ilikuwa ikilalamikiwa na wadau wengi.
Alisema
upotevu wa fedha za Serikali mwaka 2009, zilikuwa hazionekani, lakini
CAG Utouh alifanya ukaguzi ambao umesaidia fedha za madini kuongezeka.
“Ripoti
ya mwaka 2014 inaonyesha pato katika sekta hii, limeongezeka kwa
asilimia 10…takwimu zetu zinaonyesha awali kampuni za madini zilikuwa
11, sasa zimefika 60 zikiwamo kubwa na za kati,”alisema.
Utouh
alistaafu rasmi kazi Septemba 2014, baada ya kuitumikia nafasi hiyo kwa
miaka saba alipoteuliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwaka 2006.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment